Sunday, April 27, 2014

Sherehe za miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ki michezo zilifana sana pale uwanja wa Aman wakati vijana wa Kilimani City walivyowaonyesha soka safi watanzania na wanamichezo waliofika uwanjani hapo walipocheza na Turky FC timu inayovuma mjini zanzibar kwa sasa, shukurani sana kwa Dr. Abdalla Mabodi naibu waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kukatisha maadhimisha Dar na kutuunga mkono na kuongezea zawadi katika sherehe hizo ikiwemo kwa makocha wa timu hizo. matokeo ni 1-1. dakika ya 27 Chidi Zingo aliwatoka walinzi wa Turky kwa umahiri kabisa na kufunga bao safi lililonyamazisha wapenzi wengi wa Turky hadi mapumziko moja bila. kipindi cha pili Adey mchezaji wa simba ya dar aliechezea Turky ndie aliewasawaishia kama si hivyo walishalala fofofo. Kilimani City waling'ara kama Manchester City light blue t-shirts walizopatiwa na kampuni ya STONE TOWN TRADERS shukurani sana kwa kampuni hiyo. usafiri wa timu zote na wazee walioalikwa ni kampuni ya Master Mind tobacco Super Match wapo Kisiwandui kikwajuni, timu zote zilipatiwa maji ya kunywa na Super Pure maji safi yanotengenezwa Aman Industrial zone. Mwenyezi Mungu tujaalie muungano wenye neema tele.
(4 photos)
1Like · ·

Kitendo cha historia katika soka la zanzibar na Tanzania pale Kilimani City kufanya jitihada za makusudi kuwaalika wazee waliocheza soka miaka ya hamsini na sitini kwa udhamini wa SUPER MATCH MASTER MIND TOBACCO kuwapatia posho la usafiri wazee hao waliofika uwanjani Aman mechi kati ya Kilimani City na Turky FC ilipambwa na sura za wachezaji wa zamani akiwemo Keptain Ali Jabu, mzee Mkweche maalim Salum Hamdoon na wengine wengi hawa ni wachezaji walioitangaza Zanzibar kisoka na wamejumuika kuadhimisha miaka 50 ya muungano na Kilimani City inajipanga kuwaandalia Tutari ndani ya mwezi wa ramadhani kwa kuwaandalia usafiri na kufutari nao pamoja siku ya tarehe 7 July tunaamini Master Mind tobacco watawasafirisha tena waje kufutari na Kilimani City siku ya saba saba inshaallah nawe mpenzi wa Kilimani City mchango wako unakaribishwa. Wazee wa soka zanzibar tunawashukuru kwa kufika uwanjani mkituona City tulivyojipanga kuwaendeleza vijana katika soka mbunge wa jimbo la rahaleo Mh Abdalla Saadalla Mabodi tunakushukuru kwa kukaa na wazee uwanjani na kuzamisha mkono wako mfukoni kuwapatia chochote baadhi ya wazee wale ahsante sana muheshimiwa.


 
Pichani baadhi ya wachezaji wa zamani Mzee Mkweche, Salum Hamdoon na Salum Bausi.

1Like · ·

Saturday, April 26, 2014

LEO NI LEO ASIE NAMWANA AELEKE JIWE NI CITY NA TURKY AMANI MSIKOSE NA FUATILIA MATOKEO KWA ULIEKO MBALI NA MJINI MAGHARIBI TUNASHKURU STONE TOWN TRADERS KWA KUTUNG'ARISHA KWA JAZZ SAFI KABISA KUANDIKWA MIAKA 50, PIA SUPER PURE KWA KUTUPATIA MAJI YA KUNYWA KWA PAMBANO HILO NA MASTER MIND TOBACCO KWA KUTUPATIA USAFIRI WA KWENDA HUKO CITY UTAITAKA TO IS THE MATTER OF TIME. UNAWAONA VIJANA WA CITY HAO, KIT MPYA HIYO NA JINA LA MFADHILI STONE TOWN NA LUKMAN NA HASSAN WAKIPATA MAJI YA SUPER PURE INAPENDEZA KWA KWELI WAFADHILI WANAFANYA MAMBO YAENDELEE VIZURI VIWANJANI.
BY ZAINAB HAROUB AFISA HABARI KCFC.





 T- SHIRTS ZILIZOTOLEWA NA KAMPUNI YA STONE TOWN TRADERS, KUNG'ARISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

Wednesday, April 23, 2014

Mashindano makali kwa mpira wa miguu Kipwida Cup kwa mwaka 2014  ambayo inatarajiwa kuanzia tarehe 26 April kati ya Miembeni  na Njaa kali ikiwa kama wafunguzi rasmi wa mashindano hayo  katika kiwanja maalumu cha Maungani Mjini Zanzibar.
Takriban timu 18 ambazo zitashiriki katika mashindano hayo ikiwemo timu ya Kilimani City ambayo imepata nafasi bahati ya kushiriki katika mashindano hayo na itacheza na Theo kwa siku ya jumatatu tarehe 28 majira ya saa 10 jioni ambayo timu hiyo inasika kwa uzuri
Kabla ya kuchea saa 10 kutacheza timu ya Walalahoi na Red ambao wao watakuwa kama wafumbuzi wa group B kwa mzunguko wa kwanza
Na kwa tarehe 29 April itachez timu ya Tandale na Mchawi hanarangi ambayo itamaliz kwa mzunguko wa kwanza.
Mashindano hayo makali ya Kipwida Cup yanatarajiwa kukonga nyoyo za watu waliowengi kwani mashindano ya aina yake kiasi ya kwamba mshindi wa kwanza ataondoka na Ng'ombe wawili na mshindi wa pili atapata mbuzi
Hivyo mashindano hayo tunatarajia kuanza kwa salama na kumalizika kwa salama ispokuwa wapenzi wa Kilimani City inaombwa kufikwa kwa wingi kuja kuangalia timu yenu wakati itakapocheza
Kwani kutakuwa na kiingilio cha shilingi mia 500 tu

Thursday, April 10, 2014

Tarehe 26 April 2014 ni Siku ya kilele cha maadhimisho ya  miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa upande wa burudani ya mpira wa miguu kutafanyika  pambano maalum la kirafiki kati ya timu zenye mvuto Mjini Unguja Kilimani City na Turky FC.

Mpambano wa  kirafiki huo ni wa aina yake ambao utachezwa katika viwanja vya Amani Wilaya ya Mjini mnamo majira ya saa 10:00 za jioni.

Timu zote mbili zimejiandaa kumfunga mwenzake na kuonesha nani mbabe katika uchezaji wa mpira na kila moja imeshajizolea washabiki wengi.

Timu zote mbili ziko tayari kwa kuoneshana ubavu katika mechi hii itapelekea kuwa na ubishani wa hali ya juu na kuwaburudisha waTanzania kwa taifa lao kutimiza nusu karne.

Turky imejipanga kivyengine kimpira kwani toka ifanye mageuzi ya uongozi na kubadilisha usajili wakati wa dirisha dogo la usajili imepelekea kuwa wazuri zaidi kwa uchezaji wa mpira wa miguu Zanzibar.

Timu hiyo toka ifanye mabadiliko hayo kwa msimu huu wa ligi daraja la pili imeweza kufunga mechi tano mfululizo na mechi mbili za mwanzo imefunga bao sita kwa kila mechi.

Hivyo Turky ipo tayari kuadhimisha kilele cha miaka 50 ya  muungano kwa  kucheza mechi hiyo ya kirafiki na timu ya Kilimani City  ambao inasifikana kwa uzuri wa timu na wanajua mpira kwa kiwango cha juu na uongozi wa Kilimani City ukomakini kuinua hadhi ya timu yao kisoka, hivyo imetoa mvuto mkubwa kwa mpira wa miguu Unguja.

Kwaupande wa timu ya Kilimani city imejiandaa kucheza nao Turky, kwani itaongeza urafiki kwa timu ya Turky na ipo tayari kuchukua ushindi katika mechi hiyo sababu kawaida turky hupokea masomo kutuka City.

Timu za Kilimani City na Turky FC zimeahidi kutoa burudani safi kwa waTanzania katika kuadhimisha nusu karne ya muungano wa nchi mbili hizo.

Tunawaomba wapenzi wa michezo Zanzibar kuitikia wito wetu kwa kushiriki kuangalia pambano hilo la kuvutia kwa shilingi mia 500 tu, na kusherehekea miaka 50 ya Muungano wetu, udumu muungano wetu idumu Tanzania.


Tuesday, April 8, 2014

Afisa wa habari wa timu ya Kilimani City Miss Zainab Haroub amewaomba  viongozi  wa timu hiyo wameweza kukubali kuwatoa out wachezaji pamoja na uongozi wa timu  ya Kilimani City  siku ya Jumamosi tarehe 12 April  baada ya kumaliza mchezo wao wa Supper Sports na Kilimani City na kwenda kutembelea  Zanzibar Park nje kidogo ya wilaya ya Mjini ili  kuweza kubadilishana mawazo na  kuona  vitu mbali mbali vikiwemo wanyama tofauti  na vilivyomo
Afisa huyo baada ya kuona wachezaji wameweza kupoteza michezo mingi ndipo alipoamua atengeneze  mbinu  mbadala kwa kuwatoa out ili waweze kufanya vizuri katika mechi iliyobakia na hata kujiandaa kwa msimu unaofuata.
Amesema ili timu iwe nzuri basi wachezaji wanatakiwa kutoka kutembelea sehemu tofauti, hii itapelekea  wachezaji kuwa na hamu na mapenzi katika kuucheza mpira na kuboresha uhusiano baina yao na uongozi kwa ujumla.
Hivyo amesema nafasi hii ni ya kipeke kwa timu ya Kilimani City kupatiwa fursa kama hii kwani timu ligi daraja la pili hawana desturi hizo kwa hapa Zanzibar.
Afisa huyo ameamua kutumia mbinu hiyo kwa wachezaji hao baada ya kuona timu wanapoteza sana mchezo kwa michezo iliyopita ndipo alipoamua kuwatoa ili kuweza kuona mazingira na hata wanyama tofauti wakiokuwepo Zanzibar Park na kuweza kujijenga kiakili .
Uongozi umefurahishwa sana na kuona kuwa  wachezaji wameweza kutafutiwa mbinu mbadala ya kwenda kutembelea sehemu tofauti hii inaonesha jinsi gani Afisa wao wanataka kuwatengenezea mazingira mazuri kwa wachezaji hao na matokeo mazuri kwa Kilimani City hapo baadae.
Na wamesema sio Zanzibar Park tu bali hata sehemu nyenginezo kwani wachezaji wanastaki kutembea sehemu mbali mbali pindi   watakapokuwa kwenye hali ngumu ya kimpira na hata ya furaha kwani watakapo tembealea sehemu tofauti na kuona vitu mbali mbali hii itapelakea kujijenga
kiafya na kutanua akili zaidi na kujua mazingia kiujumla na kuboresha saikolojia ya timu yao na matokeo mazuri yanatarajiwa katika mechi zijazo ziwe za kirafiki au za mashindano ya kitaifa.


Afisa habari Kilimani City wa pili akiangalia City wakipambana na Shangani FC.




Saturday, April 5, 2014

Usimtukane mamba kabla hujavuka mto usemihuu umezoleka sana midomoni mwa watu na nivyema ujuwe maana yake.Nikweli kwa apewe hongera kwaalie utoa msemo huu hii inamaamna kuwa leo Kilimani City imewakata mdomo Manispaa.
 Kwakuwanyamazisha mdomo na kuwatuza kwakichapo cha mabao nane(8) kwa sufuri.Hii inaonesha kuwa Kilimani City imejipanga vilivyo na imejianda kwani mwanzo wa mchezo mnamo dakika ya kwanza, waliweza kuliona lango la goli kwa mfungaji Mussa Mshamata na dakika ya 21,38 na dakika ya 60.Dakika ya 7 na 62 mfungaji Rashid Zingo  hata hivyo dakika ya 32 aliweza kufunga Ibrahim Ameir.
Hivyo hatujakata taama ya kuingia nane bora kama inavyoweza kuonekana katika msimamo wa lligi

Shukrani kwa afisa wa habari MISS ZAINAB HAROUB pamoja na uongozi wa Timu ya Kilimani City.
POS               CLUB              PLAY                                   GD                     PTS

SHANGANI  9 8 19
2 UJAMAA 9 9 19
3 MANISPAA 10 1 17
4 VIKOKOTONI 10 5 17
5 KIJANGWANI 10 1 16
6 MZALENDO 9 2 15
7 KILIMANI CITY 10 8 14
8 MUEMBELADU 10 2 14
9 WEST COAST 9 -2 11
10 FC ROMA 9 -2 11
11 WAGUMU 9 -1 9
12 SUPERSPORTS 9 -5 7
13 GRENADA  10 -23 2


Friday, April 4, 2014

Wapenzi, washabiki na  wapizani wa timu ya Kilimani City kesho itaoneshana vilivyo siku ya jumamosi tarehe 5 April kati ya Kilamini City na Manispaa .Mchezo huo utachezwa katika  kiwanja cha Amani majira ya saa  7:30 za mchana.
Hivyo mnaombwa kufika kwa wingi kuangalia mchezo huo vijana wamejipanga vizuri kwa kucheza mechi hio kwani hawajakata taa kwa kufungwa mechi yao iliyopita kwa kufungwa bao moja lakini wamezidi kushika kasi kwa mchezo wa kesho ili kumuonesha Manispaa na kiingilio shilingi mia tano tu 500