Tarehe 26 April 2014 ni Siku ya kilele cha maadhimisho
ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, kwa upande wa burudani ya mpira wa miguu kutafanyika pambano maalum la kirafiki kati ya timu zenye
mvuto Mjini Unguja Kilimani City na Turky FC.
Mpambano wa kirafiki
huo ni wa aina yake ambao utachezwa katika viwanja vya Amani Wilaya ya Mjini
mnamo majira ya saa 10:00 za jioni.
Timu zote mbili zimejiandaa kumfunga mwenzake na kuonesha
nani mbabe katika uchezaji wa mpira na kila moja imeshajizolea washabiki wengi.
Timu zote mbili ziko tayari kwa kuoneshana ubavu
katika mechi hii itapelekea kuwa na ubishani wa hali ya juu na kuwaburudisha
waTanzania kwa taifa lao kutimiza nusu karne.
Turky imejipanga kivyengine kimpira kwani toka ifanye
mageuzi ya uongozi na kubadilisha usajili wakati wa dirisha dogo la usajili imepelekea
kuwa wazuri zaidi kwa uchezaji wa mpira wa miguu Zanzibar.
Timu hiyo toka ifanye mabadiliko hayo kwa msimu huu wa
ligi daraja la pili imeweza kufunga mechi tano mfululizo na mechi mbili za
mwanzo imefunga bao sita kwa kila mechi.
Hivyo Turky ipo tayari kuadhimisha kilele cha miaka 50
ya muungano kwa kucheza mechi hiyo ya kirafiki na timu ya
Kilimani City ambao inasifikana kwa
uzuri wa timu na wanajua mpira kwa kiwango cha juu na uongozi wa Kilimani City
ukomakini kuinua hadhi ya timu yao kisoka, hivyo imetoa mvuto mkubwa kwa mpira
wa miguu Unguja.
Kwaupande wa timu ya Kilimani city imejiandaa kucheza
nao Turky, kwani itaongeza urafiki kwa timu ya Turky na ipo tayari kuchukua
ushindi katika mechi hiyo sababu kawaida turky hupokea masomo kutuka City.
Timu za Kilimani City na Turky FC zimeahidi kutoa
burudani safi kwa waTanzania katika kuadhimisha nusu karne ya muungano wa nchi
mbili hizo.
Tunawaomba wapenzi wa michezo Zanzibar kuitikia wito
wetu kwa kushiriki kuangalia pambano hilo la kuvutia kwa shilingi mia 500 tu,
na kusherehekea miaka 50 ya Muungano wetu, udumu muungano wetu idumu Tanzania.
No comments:
Post a Comment