Tuesday, April 8, 2014

Afisa wa habari wa timu ya Kilimani City Miss Zainab Haroub amewaomba  viongozi  wa timu hiyo wameweza kukubali kuwatoa out wachezaji pamoja na uongozi wa timu  ya Kilimani City  siku ya Jumamosi tarehe 12 April  baada ya kumaliza mchezo wao wa Supper Sports na Kilimani City na kwenda kutembelea  Zanzibar Park nje kidogo ya wilaya ya Mjini ili  kuweza kubadilishana mawazo na  kuona  vitu mbali mbali vikiwemo wanyama tofauti  na vilivyomo
Afisa huyo baada ya kuona wachezaji wameweza kupoteza michezo mingi ndipo alipoamua atengeneze  mbinu  mbadala kwa kuwatoa out ili waweze kufanya vizuri katika mechi iliyobakia na hata kujiandaa kwa msimu unaofuata.
Amesema ili timu iwe nzuri basi wachezaji wanatakiwa kutoka kutembelea sehemu tofauti, hii itapelekea  wachezaji kuwa na hamu na mapenzi katika kuucheza mpira na kuboresha uhusiano baina yao na uongozi kwa ujumla.
Hivyo amesema nafasi hii ni ya kipeke kwa timu ya Kilimani City kupatiwa fursa kama hii kwani timu ligi daraja la pili hawana desturi hizo kwa hapa Zanzibar.
Afisa huyo ameamua kutumia mbinu hiyo kwa wachezaji hao baada ya kuona timu wanapoteza sana mchezo kwa michezo iliyopita ndipo alipoamua kuwatoa ili kuweza kuona mazingira na hata wanyama tofauti wakiokuwepo Zanzibar Park na kuweza kujijenga kiakili .
Uongozi umefurahishwa sana na kuona kuwa  wachezaji wameweza kutafutiwa mbinu mbadala ya kwenda kutembelea sehemu tofauti hii inaonesha jinsi gani Afisa wao wanataka kuwatengenezea mazingira mazuri kwa wachezaji hao na matokeo mazuri kwa Kilimani City hapo baadae.
Na wamesema sio Zanzibar Park tu bali hata sehemu nyenginezo kwani wachezaji wanastaki kutembea sehemu mbali mbali pindi   watakapokuwa kwenye hali ngumu ya kimpira na hata ya furaha kwani watakapo tembealea sehemu tofauti na kuona vitu mbali mbali hii itapelakea kujijenga
kiafya na kutanua akili zaidi na kujua mazingia kiujumla na kuboresha saikolojia ya timu yao na matokeo mazuri yanatarajiwa katika mechi zijazo ziwe za kirafiki au za mashindano ya kitaifa.


Afisa habari Kilimani City wa pili akiangalia City wakipambana na Shangani FC.




No comments:

Post a Comment