Thursday, March 20, 2014

Kivumbi kikali  kilitimuka katika uwanja wa Amani wilaya ya Mjini kati ya Kilimani City na Shangani waliweza kuoneshana ubavu uwanjani hapo.
Mchezo huo ulichezwa majira ya saa saba na robo hapo ndipo timu ya Kilimani City waliweza kukitawala kipindi chote cha kwanza hatimaye dakika za lala salama ililiona lango la Shangani ndani ya dakika ya 44 mototo alielelewa na Shangani wenyewe Rashid Zingo (Chidi Zingo) aliweza kuitoroka ngome ya Shangani na kuukwamisha mpira wavuni hadi kumalizika kwa kipindi cha kwa bao moja kwa sifuri. kabla ya goli hilo mwamuzi Shaaban alimtoa Kocha wa Kilimani City kwenye maeneo ya viongozi baada ya kumtolea maneno ambayo hayakubaliki mchezoni. watu walikuwa ni wengi na mpira ulikuwa wa kasi na kusisimuwa, ingawa City walipoteza nafasi nyingi za wazi na wanazijutia kwa ukweli.
Kwa kipindi cha pili mchezo ulikuwa mkali kwa timu zote mbili kwani kila mmoja alikuwa anahamu ya kumuonesha mwezake ubavu na hadi dakika ya 72 Shangani waliweza kurejesha bao na kwa mfungaji wao Ismaili Kasim. Hadi mwisho wa mchezo City 1 na Shangani 1.
Mpira kwa ujumla ulikuwa mzuri sana na tunawapongeza vijana wetu wa Kilimani City kwa kuonyesha kandanda safi watu roho inapenda.
Tunawashukuru wadhamini wa Kilimani City Prize Insurance Broker na Super pure kwa kuendelea kuidhamini timu ya City kwa kuwapa seti ya jazi na maji ya kunywa kwa mechi sita zilizobaki.
Shangani inaongoza kundi B kwa kujikusanyia point 16 kwa michezo nane iliyocheza City tupo nafasi ileile ya nane kwa point zetu 11 tumebakisha mechezo minne tu nafasi ya kuingia nane bora ni finyu kwetu ila tunaendelea kupambana vikali, kwa kujivinjari katika mazowezi.
Muda wa mashindano hayo wa saa nane mchana kutokana na uchache wa viwanja ni changamoto kwa vilabu vyetu ni mgumu sana na nyasi bandia zinasumbua kama jua linakuwa kali, Serikali iwekeze kwa kuengeza viwanja kwa kuinua hadhi ya soka Zanzibar.
Aidha tuwawapongeza mashabiki wote waliofika uwanjani kuhudhuria pambano letu uwepo wao unaonyesha heshima kubwa kwetu kwa kukubali kazi wanayoifanya vijana wetu.
Kilimani City itajitupa uwanjani tena siku ya Jumatatu ya tarehe 31 Machi hapo hapo uwanja wa Amaan Stadium dhidi ya timu ya Ujamaa. Kesho tarehe 21 Machi ni Ujamaa na Kijangwani Amani.

Fuatilia na baadhi ya picha hapo chini:





Washambuliaji wa Kilimani City wakiliandama lango la wapinzani wao Shangani FC.
Kocha Kwimbi aliesimama jukwaani akitafuta sehemu ya kukaa baada ya kutolewa na mwamuzi wa pambano hilo Shaaban baada ya kurusha maneno dhidi yake.


Chidi Zingo akishangiria mara tu ya kuukwamisha mpira wavuni na kufanya City kuongoza baada ya dakika ya 44 kipindi cha kwanza.


Chidi Zingo wanne kutoka kulia mfupi wao akishangiria na wachezaji wenzake tisa baada ya kutikisha nyavu za Shangani FC.




Lukman Ayoub akinywa maji ya Super Pure udhamini wa kampuni ya Safari Company Ltd wa pale Aman Industrial Zone akiwa na Hassan alieikamata chupa ya Super Pure na jazi walizodhaminiwa na Prize insurance Broker baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Kocha msaidizi Seif Hafidh Suleiman (Waziri).



Shukurani kwa Afisa Uhusiano Miss Zainab Haroub na idara ya Habari Kilimani City.


















































No comments:

Post a Comment