Saturday, March 29, 2014

LIGI daraja la pili inazidi kushika kasi  kwa Wilaya ya mjini, kwa mzunguko wa kumi(Round10) ambayo kwa timu ya Kilimani city inatarajiwa kuchezwa na Ujamaa siku ya Jumatatu tarehe 31Machi majira ya 7:30 za mchana katika uwanja Amani  na kwa upande wa Manispaa na Kijangwani siku hiyo hiyo watacheza katika uwanja wa Mao us tung saa 8:00 za mchana.

Kabla ya mechi ya Kilimani City na Ujamajaa siku ya Jumamosi  tarehe 29 Machi timu ya Vikokotoni imeichabanga FC Roma magoli matatu kwa moja mchana katika uwanja wa Amani.na kuchupa hadi nafasi ya pili kwa kujikusanyia point 17 kibindoni Jumapili tarehe 30 majira ya saa7:30 watacheza Shangni na Mzalendo  katika uwanja wa Amani  na saa 8:00 watacheza Muembeladu na West coast pale Mao

Na kwakumalizikia kwa mzunguko wa kumi (Round 10) itakuwa siku ya Jumanne tarehe 1 April mwaka 2014 watamalizia kwa timu ya Super Sports na Grenada.
Kwaupande wa msimamo wa ligi hiyo Kundi B ni kama ufuatavyo:

           PS      CLUB            PLAY          GD          PTS
1   MANISPAA 8 12 17
2  VIKOKOTONI 10 5 17
3  UJAMAA 8 8 16
4  SHANGANI  8 7 16
5  MZALENDO 8 3 15
6  KIJANGWANI 9 -2 13
7  KILIMANI CITY 8 1 11
8  ROMA 9 -2 11
9  MUEMBELADU 9 1 11
10  WEST COAST 8 -1 11
11  WAGUMU 9 -1 9
12  SUPERSPORTS 8 -12 4
13  GRENADA  9 -16 2







   Shukurani kwa Afisa wa habari Miss Zainab Haroub na idara ya habari ya  Kilimani City  kwa kuweza kuwajuza jamii kwa kila kinachoendelea katika timu yao.


Afisa uhusiano Kilimani City Miss Zainab Haroub wa pili akifuatilia pambano kwa umakini kabisa

Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Haji Chura wa kwanza kushoto akitafakari maendeleo ya soka ya wilaya yake akiwa na wadau wa soka wa wilaya hiyo uwanjani Aman.

No comments:

Post a Comment